@mtabe-innovations
Kozi hii ya Python Language imeandaliwa kwa ajili ya wanaoanza kujifunza programu hii. Hapa utapata ufahamu wa kina kuhusu matumizi ya Python kuanzia hatua za awali mpaka kuwa mtaalamu wa kutumia lugha hii katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo. Python ni lugha muhimu sana kwa wale wanaotaka kujifunza programu za kompyuta na kutengeneza software.
@mtabe-innovations
Kozi hii itakufunza kwa undani namna ya kutumia Microsoft PowerPoint kuanzia mwanzo hadi mwisho. Utajifunza mbinu za kitaalamu za kuunda mawasilisho ya kuvutia, kutumia zana za kisasa za uhariri, na kuwasilisha kwa ufanisi mbele ya hadhira yoyote. Kozi hii ni muhimu kwa kila mtu anayetaka kuboresha ujuzi wake katika mawasilisho, iwe kwa kazi, masomo, au biashara. Baada ya kumaliza, utapata cheti kinachoonyesha ufanisi wako na maandalizi yako kwa ufanisi.
@mtabe-innovations
Hii kozi imefundishwa kuanzia ngazi ya msingi mpaka ngazi ya utaalamu. Mwisho wa kozi utaweza kutumia huu ujuzi kuweza kuandika nakala mbali mbali kama barua, risiti, mchapisho kama mitihani. Huu ujuzi unaweza kutumika maofisini, shughuli binafisi pia kujiingizia kipato au ajira kama kufanya kazi stationary au kua secretary wa taasisi au ofisi.
@mtabe-innovations
Hii kozi ya Excel imefasisirwa kwa lugha ya Kiswahili na mtalamu wa Data yaani (Data Analyst). Kozi hii itakufunza kuanzia msingi wa chini mpaka kuweza kua mtaalamu wa kutumia software ya Excel vizuri. Excel ni muhimu sana katika kutunza kumbukumbu za mahesabu kama madukani, ofisini pia kuandaa risiti na invoice kwa wateja.
@mtabe-innovations
Kupitia kozi hii utajifunza kuongea na kuandika kiingereza fasaha kutoka kwa mtaalamu wa lugha ya kiingereza. Kozi imegawanyika katika vipindi 16, vyote vipo kwenye mfumo wa videos na kwa kiswahili. Zaidi ya hapo, utaunganishwa kwenye group ambalo unaweza kuuliza swali muda wowote kupata msaada.